Balozi wa umoja wa Ulaya hapa nchini Tanzania Bw. Filiberto Sebregondi
Mwenyekiti wa mfuko wa sekta binafsi nchini Dkt. Regnald Mengi amesema itakuwa vigumu kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kukuza uchumi kama hazitadhibiti tatizo sugu la Rushwa linaloendelea kujikita katika sekta mbalimbali.
Dr. Mengi ameyasema hayo jijini Arusha katika hafla ya utiaji saini mkataba wa msaada wa Euro Milioni 2.3 zilizotolewa na Jumuiya ya Ulaya kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika ukanda wa bahari ya Hindi.
Dr. Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP amesema tatizo la rushwa limeendelea kushika kasi na udhibiti wake unaendelea kuwa mgumu kutokana na utaratibu unaotumika kulishughulikia ambao umejikita zaidi kwa wanaotoa na kwa watu wadogo wadogo .
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la wafanyabiashara Afrika Mashariki Bw. Felexs Mosha na mwenyekiti wa watendaji wakuu wa makampuni nchini Bw Ally Mafuruku Wamesema pia nchi za wanachama wa jumuiya hiyo zinakabiliwa na tatizo la gharama kubwa za uwekezaji na ukosefu wa taarifa muhimu.
Naye naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia fedha na utawala Jean Cloude amesema msaada huo wa Jumuiya ya Ulaya utasaidia kuimarisha ulinzi hasa eneo la bahari ya Hindi ,
Balozi wa umoja wa Ulaya hapa nchini Bw. Filiberto Sebregondi pamoja na kuelezea azma ya Jumuiya ya Ulaya ya kuendelea kuisadia Jumuiya ya Afrika Mashariki amesema pamoja na changamoto zinazojitokeza zikishughulikiwa upo uwezekano.
Msaada huo wa Euro Milioni 2.3 kutoka Jumuiya ya Ulaya (EU) ni mwendelezo wa kampeni za Jumuiya hiyo kuisadia Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kwa
kipindi cha mwaka 2010 kiasi cha Euro Milion 37.5 zimetolwa.