Jumatano , 6th Jul , 2016

Mufti Mkuu Sheikh Abubakar Zuberi amewataka waislamu nchini kuenda wema na kujiepusha na maovu baada ya kumalizika kwa Mwezi Mkukufu wa Ramadhani.

Mufti ameyasema hayo leo katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es salaaam ambapo waislamu nchini wameungana na wenzao kufanya ibada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumalizika salama kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

''Leo ni siku muhimu, nawataka waislamu wote tujiepushe na maovu kwani kufanya kosa leo ni utakumbana na hukumu siku ya kiama, tuitumie siku ya leo kumrishisha mwenyezi Mungu kwa kufanya mambo mema''Amesema Mufti''- amesema Mkuu Sheikh Abubakar Zuberi.

Aidha Sheik Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum amesema kwamba waislamu wanapaswa kupendana kama walivyofanya kwenye mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni pamoja na kutoa sadaka na kutunza amani ya nchi.