
Mawimbi ya Tsunami
Mwakilishi huyo ametoa onyo hilo hii leo ikiwa ni siku ya maadhimisho ya kimataifa ya mara ya kwanza kuhamasisha dunia kuhusu athari za tsunami,
Akizungumza Jijini New Delhi, India katika mkutano wa ukanda wa Asia wa mawaziri wanaoshughulikia upunguzaji wa hatari ya majanga Bwana Glasser amenukuu ripoti mbili za hivi karibuni zinazoonesha kuwa matukio ya tsunami yanaweza kutokea katika maeneo mengi duniani.
Hata hivyo amesema Ulaya na Amerika ziko hatarini sambamba na nchi zinazozunguka Bahari ya India na Pasifiki.
Naye mwandishi mkuu wa moja ya tafiti hizo, Profesa Fumihiko Imamura amesema ni muhimu kuhamasisha dunia kuhusu athari za tsunami na watu lazima waelewe cha kufanya na wapi pa kwenda mara moja kengele ya tahadhari inapotolewa.