Alhamisi , 8th Sep , 2016

Hospitali ya Benjamin Mkapa ya UDOM, Mjini Dodoma imeanza kutoa huduma ya ugonjwa wa saratani kwa watoto wadogo kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la marafiki wa watoto wanaoishi na saratani nchini.

Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo UDOM

Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. James Charles, amesema kuwa hospitiali hiyo itatoa huduma kwa kutumia taarifa za wagonjwa kutoka katika vituo vya afya.

Dkt. Charles amesema kuwa kuanza kwa kutolewa kwa huduma hiyo kutasaidia wakazi wa Dodoma na mikoa ya kati kuanza kupata matibabu hayo kwa wakati huku akizitaja dalili za saratani kwa watoto wadogo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika hilo la marafiki kwa watoto wanaoishi na saratani, Janeth Malone, amesema kuwa tafiti zinaonesha kuwa zaidi ya watu elfu 40 kila mwaka wanapata saratani nchini Tanzania.