Alhamisi , 22nd Sep , 2022

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 22, 2022, bungeni jijini Dodoma, amepata kigugumizi kidogo wakati alipotakiwa kujibu swali la mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina.

Kushoto ni Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba na kulia ni Mbunge Luhaga Mpina

Swali la mbunge Luhaga Mpina lilitaka kujua sababu zilizopelekea kesi 1,097 za kodi za muda mrefu, zenye thamani ya Trilioni 360 na dola za Marekani milioni 181.4 kutoamuliwa hadi sasa, ambapo awali lilijibiwa na Naibu Waziri wa Fedha na halikumridhisha mbunge huyo na ndipo Spika wa Bunge akaingilia kati.

"Mhe. Spika, Trilioni 360 hazipo kwenye 'TRAB' na 'TRAT' ni kitu tofauti kabisa, hazipo kwenye mashauri ya kikodi ya, ya, ya, ya ya ya ya ya ya 'TRAB na TRAT' hili ni jambo mahususi lililokuwepo kwenye mzozo wa serikali na Barrick,", amejibu Waziri Nchemba.

Tazama video hapa chini