
Vifaa vya waganga
Mkuu huyo wa wilaya ya Itilima, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani hapo, amesema kuwa mganga yeyote wa jadi anayetumia viungo vya wanyamapori pasipo usajili, anakiuka sheria za nchi, hivyo ni lazima mwenye navyo asajiliwe vinginevyo atakabiliwa na shinikizo la sheria.
"Hizi nyara huna sababu ya kukaa nayo kwa hofu njoo usajili ili ukae nayo, sisi kama ambavyo tulivyoweka mkakati wetu kwamba habari za vitisho kwa waganga wa tiba asilia wale wanaofanya kazi kwa mujibu wa sheria itabaki kuwa ndoto, inabidi mpate usajili ili mfanye kazi zenu kwa uhuru", amesema DC Kilangi.