Jumatatu , 4th Feb , 2019

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema uamuzi wa CCM kuwateua madiwani waliotoka upinzani kugombea tena nafasi hizo ulikuwa ni moja ya mikakati ya ushindi wa kurejesha kata zilizokuwa upinzani kuwa mikononi mwa chama tawala.

DC Richard Kasesela

Akizungumza katika kongamano la miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM lililofanyika Iringa, wakati akijibu hoja iliyoibuliwa na wajumbe ambao walidai kusikitishwa na uamuzi wa kuwapokea madiwani kutoka upinzani kisha kupitishwa kugombea tena nafasi hizo.

Kasesela ameeleza kwamba, “tuliamua waliohamia CCM kutoka upinzani wagombee ikiwa ni moja ya makubaliano ya wao kuhamia na tulikubali kwa sababu ulikuwa ni mpango wa chama kuhakikisha kata zote zinarudi CCM".

Hata hivyo www.eatv.tv ilipomtafuta Kasesela kufafanua kauli yake kuhusu wapinzani waliohamia CCM kwamba si kutokana na kuunga juhudi za Rais Magufuli kama jinsi ilivyoelezwa awali, hakupokea simu yake.