Akizungumza kwenye Kampeni za kumnadi Mgombea Ubunge wa Kinondoni Salum Mwalimu Ole-Sosopi amesema kwamba kilichowafanya kususia uchaguzi mara ya kwanza ni kwamba hakukuwa na faida kubwa ya kupatikana kiongozi kwa wananchi wasio na hatia kwa kumwaga damu.
Ole-Sosopi amesema kwamba baada ya kususia uchaguzi ambao uligomewa kupelekwa mbele sasa wamegundua kuwa "dawa ya muhuni ni kuwa muhuni zaidi hivyo ifahamike na iwekwe rekodi kuwa CHADEMA tumerudi na kushiriki na kufanya uchaguzi".
Mbali na hayo Ole-Sosopi ameongeza kuwa hataki chama chake au kingine kisipendelewe bali waachwe wabishane kwa hoja na mwishowe wananchi waachiwe kufanya maamuzi.
CHADEMA walitangaza kugomea uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 13 kwa madai mbalimbali ikiwepo kufanyiwa hujuma za wazi katika uchaguzi uliofanyika Novemba 26 huku Tume ya uchaguzi ikilalamikiwa kutofanyia kazi malalamiko hayo.


