Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi,( CUF), Profesa Ibrahim Lipumba akihutubia wananchi wa Handeni.
Profesa Lipumba amesema hayo wakati akiomba kura kwa wananchi wa kata ya Kwakonje wilayani Handeni Mkoani Tanga ambapo amesema kuwa kupata maji safi na salama ni haki ya Mtanzania yeyote na ndio chanzo cha maendeleo ya taifa.
''Ndugu zangu tunaomba kura zenu ili tuweze kuwamalizia hili tatizo la maji ambalo ccm wameshindwa kulitatua tokea kujitawala kwake tunawaomba kura zenu tuweze kuhakikisha kila kijiji kina zahanati na kituo cha afya chenye waganga wakutosha na dawa,'' alisistiza Prof.Limumba
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa CUF Taifa, amelaani vikali kitendo cha tabia ya Katibu wa CCM, wilaya ya Handeni, kuwatishia wagombea na wafuasi wa CUF ili wasifanye siasa zao na kutaka kuwanunua baadhi ya wagombea wao na kuahidi atakwenda kumuona Rais Magufuli na katibu mkuu wa CCM Dkt. Bashiru ili waweze kumuwajibisha kiongozi huyo.
Mgombea urais huyo amesema chama cha CUF,kinahitaji kufanya siasa za kistaarabu hawako tayari kumvumilia yeyote atakayejaribu kuwakwamisha kufanya siasa zao kwa maslahi ya wananchi.
''Tunahitaji tufanye siasa za kistaarabu hatuhitaji maisha ya kutishana nitamueleza Magufuli na katibu wao Dokta Bashiru Ally ili amuwajibishe katibu wake wa wilaya ya Handeni anayewatishia wafuasi wa CUF wasifanye shughuli za kisiasa,'' alisisitiza Profesa Lipumba.