Kauli hiyo inakuja Mara baada ya uwepo wa malalamiko mbalimbali ya madereva wanaosafirisha mizigo masafa Marefu kuwa Baadhi ya vipengele havifuatwi na waajiri wao ikiwemo mikataba licha ya Serikali kuweka wazi Sheria na utaratibu.
EATV imefanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa chama cha wafanyakazi wa maroli Tanzania(CHAMAWATA) Greyson Wimile Ambaye ameweka uhalisia ulivyo katika suala la mikataba.
"Ni kweli ndugu mwandishi tunachangamoto ya mikataba na inayotolewa mingi haikidhi masharti ya Ile iliyotolewa na serikali lakini waajiri bado wamekuwa sio waaminifu katika hilo."
Amesema huko nyuma serikali tayari iliweka utaratibu wa mikataba akiiomba wizara ya kazi kupitia maafisa wake kupita katika Makampuni yote kuona Kama yanafuata miongozo iliyowekwa.
Sera ya usafirishaji bado sio rafiki unajua uchumi unabebwa kwa kikubwa na sekta hii, madereva wanabeba uchumi utakumbuka kwenye kipindi Cha Covid 19 Madereva wameendelea kupambana kusafirisha mizigo."
Hata hivyo bw Greyson ametoa Rai kwa madereva,kutimiza wajibu wao Sambamba na waajiri wao kwa kuwa Uchumi kwa kiasi kikubwa umebebwa na sekta ya usafirishaji.
"Rai yangu kwa serikali niiombe Wizara ya kazi na ajira kuhakikisha inapitia maagizo iliyoyatoa kwa wamiliki Kama yanatekelezwa".