Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe
Akizungumza jana katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho mwenyekiti wa taifa wa chama hicho Mhe. Freeman Mbowe amesema kuwa anahisi wakati viongozi hao wakishikiliwa uchaguzi utaishwa wakati makada wao wakiwa kizuizini.
Mhe Mbowe amesema kuwa hatua ya kukamatwa viongozi hao ni hujuma za kisiasa zinazoendelea ambapo pia kumekua na mikakati ya kuzigawa manispaa wanazoziongoza ili Chama cha Mapinduzi kiweze kuchukua nafasi katika halmashauri mpya.
Wabunge wanaoshikiliwa na polisi mpaka sasa ni Mbunge wa Jimbo la Kawe Mhe. Halima Mdee. Mbunge wa Ukonga Mhe. Mwita Waitara pamoja na madiwani wawili lakini pia Mbunge wa jimbo la Ubungo Mhe. Said Kubenea anaendelea kutafutwa na jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano zaidi.