Jumatatu , 3rd Aug , 2015

Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini Tanzania CHADEMA kimesema hakipo tayari kumsubiri Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Wilbrod Slaa kutokana na kutokubaliana maamuzi mbalimbali yaliyofanywa hivi karibuni na chama hicho ikiwemo suala la mgombea

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe wakati wa ufunguzi wa kikao cha Kamati Kuu ambapo amesema wamefanya vikao vya makubaliano na Katibu wa chama hicho na yeye amekubali kukiacha chama kiendelee na majukumu ya shughuli za uchaguzi.

Aidha, Mhe. Mbowe amesema tofauti zilizopo hazifanyi shughuli za chama kutetereka na kuwa kwa sasa wamejipanga katika kusimamia mustakabali wa maendeleo ya nchi kwa kuhakikisha wanaweka wagombea ambao watasimamia Ilani ya Chadema katika kuleta mababadiliko katika nchi.

Mbowe ameongeza kuwa bado wanatamani kufanya kazi na Dkt Slaa na wanaamini kuwa ni muelewa na akitafakari na kuona ni vyema kurudi bado nafasi yake ipo na kuwa suala la uongozi katika chama hicho ni suala muhimu na lenye kuheshimiwa kwa mustakabali wa maendeleo ya chama.

Hata hivyo amesisistiza kuwa maamuzi hayo hayakufanyika na kiongozi mmoja katika chama bali makubaliano ya pamoja na wajumbe wa kamati kuu wa CHADEMA wameridhia kusimama kwake na kuacha mchakatop wa uchaguzi mkuu kuendelea.