Jumatatu , 30th Jan , 2017

Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, Moussa Faki Mahamat, leo amechaguliwa na viongozi wa Afrika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kuwa Mwenyekiti mpya wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika.

Moussa Faki Mahamat

Bw. Mahamat ameshinda kwa kura 28 dhidi ya 24 za mpinzani wake wa karibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Bi. Amina Mohamed, ambaye walichuana naye vikali.

Anachukua wadhifa huo kutoka kwa Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma wa Afrika Kusini . Bw. Mahamat amewahi pia kuwa Waziri Mkuu wa Chad na mwanadiplomasia anayeheshimika akizungumza lugha tatu, Kiingereza, Kifaransa na Kiarabu.

Wakati huo huo, Rais wa Guinea, Alpha Conde, amepokea kijiti cha Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kutoka kwa Rais Idris Derby wa Chad.

Zoezi la upigaji kura likiendelea