Jumapili , 9th Jan , 2022

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza mchakato wa kumpata spika mpya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambao utaanza Januari 10, 2022 kwa wenye nia kuchukua fomu, na kuhitimishwa mwisho wa mwezi kwa wabunge wa chama hicho kupiga kura za kumpitisha mgombea. 

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Shaka Hamdu Shaka

''Kuanzia tarehe 10-15, litafanyika zoezi la kuchukua na kurejesha fomu kwa wabunge wa CCM kuomba kuteuliwa na chama kuwania kiti cha Spika'' - Shaka Hamdu Shaka, Katibu Mwenezi.

''Tarehe 17, 2022 sekretarieti ya Halmshauri Kuu ya Taifa itakutana kwaajili ya kujadili wagombea na kuishauri Kamati Kuu juu ya wagombea ambao wamejitokeza kuomba kiti cha uspika'' - Shaka Hamdu Shaka, Katibu Mwenezi.

''Tarehe 18-19 kutakuwa na kazi ya kuchuja na kufanya uteuzi wa mwisho ambapo kamati kuu ya Halmashauri kuu itafanya kazi hiyo'' - Shaka Hamdu Shaka, Katibu Mwenezi.

''Kuanzia tarehe 21-30, katika siku hizo, Cocas ya Chama ya wabunge wa CCM itapiga kura kumpata mbunge ambaye atakwenda kusimama bungeni kwaajili ya kuomba kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania'' - Shaka Hamdu Shaka, Katibu Mwenezi.

Tazama hapo chini Shaka akieleza