Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wanafunzi wanaolala kwenye bweni hilo wameeleza kuwa wamepoteza vitu vyao kama madaftari, godoro na nguo huku wengine walikuwa kwenye maandalizi ya kufanya mitihani.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kagera Mzamilu Hassan, amesema kuwa hakuna kifo wala majeruhi na uchunguzi wa kubaini chanzo cha moto huo bado unaendelea.
Hili ni tukio la pili bweni la shule hiyo kuungua moto ndani ya mwaka huu ambapo tukio la kwanza liliunguza bweni la wavulana.