Alhamisi , 26th Jun , 2014

Serikali ya Tanzania imewasilisha bungeni azimio la kuridhia itifaki ya kuanzisha umoja wa fedha wa jumuia ya Afrika mashariki,ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuelekea kwenye matumizi ya sarafu moja kwa nchi za jumuia hiyo.

Mbunge wa Ubungo John Mnyika.

Akiwasilisha bungeni azimio hilo jana naibu waziri wa fedha Adamu Malima amesma kuwa majadiliano ya itifaki hiyo yalianza Jamuari mwaka 2011 na kukamilika Julai mwaka 2013.

Waziri Malima amesema itafaki hiyo ilidhinishwakatika ngazi zote za jumuia hiyo ambazo ni baraza la mawaziri wa sekta ya umoja wa fedha, mkutano mkuu wa dharura wa 27 wa baraza la mawaziri la jumuia ya Afrika mashariki lililofanyika Julai 2013 na baraza la sekta ya sheria na katiba.

Hata hivyo baadhi ya wabunge, akiwemo mbunge wa Ubungo John Mnyika alionyesha wasiwasi juu ya azimio hilo kwa madai kuwa huenda likaleta mgogoro wa kikatiba huku wale wa kutoka chama tawala wakitetea umuhimu wa Tanzania kuridhia azimio hilo ingawa kwa uangalifu mkubwa.