Alhamisi , 6th Feb , 2025

Madereva bodaboda mkoani Dar es Salaam wamelalamikia tabia isiyofaa ya baadhi ya abiria wao hususani wanawake wanaowalaghai kwa kuwataka kingono badala ya kuwapa malipo yao waliyokubaliana.

Uchunguzi wa EATV umebaini kuwepo malalamiko ya baadhi ya madereva bodaboda mkoani hapa ambao wanakiri kuwepo kwa mitego hiyo ya kubadilishiwa ngono dhidi ya nauli ya boda ambayo mara nyingi huwa ya umbali unaoweza kugharimu kati ya shilingi 1500 mpaka shilingi 2000 za kitanzania.

Bw. CHARLES KOMBOLE ni dereva bodaboda mkoani Dar es salaam na hapa anakiri kwamba ameshawahi kukutwa na hali hii baada yam dada mmoja kumwambia ampeleke Kawe kutokea Makumbusho.

OSMAN IDDI ambaye pia anafanya kazi hii ya bodaboda hapa mkoani Dar es salaam na yeye pia anakiri kuwahi kujaribiwa kuingizwa kwenye mtego huo japo ametujuza kwamba aliushinda anasema kwamba vishawishi hivi hushamiri sana nyakati za usiku na  anasema kuwa kuna baadhi ya vijana boadboda bila kujali afya zao  huingia kwenye mtego huo bila kinga.

Kwa sasa huku mitaani kuna tetesi zinazosemekana kwamba dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI huenda zisipatikane kiurahisi sana, kutokana na Rais wa sasa wa marekani Donald Trump kuja na sera inayozuia misaada Afrika, jambo hili wananchi wanasubiria kauli ya serikali , huku tabia hatarishi kama hizi za wadada wanaotuhumiwa kujiachia bila kujali afya, zikiichagiza tetesi kwamba fanya ufanyayo ila ARV zinaweza kuleta matata ya upatikanaji na taarifa hizi bodaboda haw awanazo.

Wafuatiliaji wetu katika mitandao ya kijamii ukiwemo X zamani ukijulikana kama twiter wengi wameonyesha kushangazwa na taarifa hii, huku wakijiuliza kwani hao bodaboda wnalazimishwa? Lakini ukweli ni kwamba suala hili ni kubwa sana kwa bodaboda wa hapa mjini Dar kiasi cha kulizungumza pale wanapofanya vikao vyao.