
Bill Clinton na mkewe Hillary ni miongoni mwa viongozi wa ngazi ya juu waliotumiwa hati ya kisheria wakihitajika kufika mbele ya Kamati ya Bunge inayoendeleza uchunguzi kumhusu Jeffrey Epstein aliyefungwa jela kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono uliohusisha pia watoto.
James Comer, mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi ya Bunge, alitoa hati za mahakama kwa familia ya Clinton na watu wengine wanane.
Kamati ya Bunge inayohusika na uchunguzi huo, inatafuta taarifa zaidi juu ya historia ya Epstein, baada ya Rais Doanld Trump kufuta ahadi ya kufichua mafaili ya kesi hiyo.
Shinikizo limekuwa likizidi kwa Rais Trump kuruhusu kufichuliwa kwa taarifa zaidi kuhusu sakata la Eipsten aliyefia gerezani mwaka wa 2019.
Uamuzi huo ulisababisha hasira kati ya wafuasi wa Trump na baadhi ya waliberali, waliokataa kukubali taarifa ya Idara ya Sheria kwamba hakukuwa na "orodha ya wateja" katika faili za Epstein.
Kamati hiyo pia imeitisha idara ya sheria yenyewe kutoa rekodi zinazohusiana na Epstein.