Jumanne , 1st Nov , 2016

Bei ya zao la chai katika mnada wa Mombasa imeongezeka kwa mara ya kwanza wiki iliyopita, na kufufua matumaini kwa wakulima juu kuimarika kwa mapato katika mwaka huu wa fedha.

Shamba la chai

 

Bei ya kilo moja ya majani ya chai katika mnada huo imeuzwa kwa shilingi 229 za Kenya ikiwa ni ongezeko la asilimia 6, ikilinganishwa na shilingi 217 bei ya zamani.

Hata hivyo bei hiyo bado ni ya chini ikilinganishwa na mauzo ya bei ya chai katika kipindi kama hicho mwaka jana ambapo kilo moja ya majani ya chai iliuzwa kwa shilingi 298 za Kenya.