Jumapili , 1st Nov , 2020

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi,(CCM), Dk.Bashiru Ally, amewataka viongozi wa chama hicho waliochaguliwa katika ngazi za  Udiwani,Ubunge na Wawakilishi kuzingatia nidhamu ya chama na uwajibikaji.

Akizungumza hii leo Novemba 1,2020,Dk. Bashiru, amesema kuwa wanao mfumo  kwenye jumuiya zao za chama na kamati za siasa za ngazi zote ambazo zitasimamia na kudai kuwa deni walilonalo ni kuhakikisha wanafanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

''Kwa mara ya kwanza chama chetu kimeingia na kumaliza uchaguzi kikiwa na umoja na mshikamano tukiwa tunaheshimiana na kusimamiana niwaombe wana CCM, wasianze kusherehekea ushindi huu kana kwamba kazi imeisha ila kiukweli kazi ngumu imeanza''amesema Dk. Bashiru Ally

Aidha amesema siri kubwa ya ushindi walioupata  ni umoja wao na kuongeza kuwa ushindi huo ni kutokana na kazi nzuri waliyoifanya katika miaka mitano iliyomalizika.