
Rais Magufuli akimpigia simu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Doto james siku ya Jumanne Julai 16, 2019.
Akiwa jijini Mwanza leo Julai 20, 2019, Naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Elias Kwandikwa amepokea makontena 10 ya vifaa vya ujenzi huo wa cherezo pamoja na ukarabati wa meli za MV Butiama na MV Victoria.
Malori yaliyobeba Makontena yakiwasili Mwanza leo.
Baada ya kubaini makotena hayo yamekwama Mwanza, Rais Magufuli alimpigia simu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na kumtaka ahakikishe taratibu zote zinakamilika kwaajili ya makontena hayo kufika Mwanza kwa wakati.
Aidha makontena 10 yaliyofika leo Mwanza na kupokelewa na Naibu Waziri Kwandikwa ni sehemu ya makontena 56, ambayo awali yalikuwa yamekwama Dar es Salaam.
#VIDEO Rais Magufuli mapema leo alipompigia simu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha. pic.twitter.com/M3u0Ie465i
— East Africa TV (@eastafricatv) July 16, 2019