
Jackline Mkonyi, aliyejeruhiwa na mume wake
Taarifa hiyo imetolewa leo Mei 28, 2023, na Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo, na kusema mtuhumiwa wanaendelea kumhoji na pindi upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.
Aidha ametoa onyo kwa baadhi ya watu wachache wanaofanya vitendo vya ukatili katika familia zao ama sehemu nyingine kuacha mara moja kwani hawatasita kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria.
Lakini pia amewaomba wananchi popote walipo wasifumbie macho vitendo viovu na waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha wanatoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao ili kukomesha matukio hayo katika jamii.