Jumatano , 11th Aug , 2021

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, linamshikilia Mabula Joseph (31), Mkazi wa Kata ya Inyala, kwa tuhuma za kumuuwa mpenzi wake aitwaye Jema Mela (36), aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Inyala kwa kumcharanga na mapanga kisha na yeye kujaribu kujiua kwa kunywa sumu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei

Akizungumza hii leo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ulrich Matei, amesema tukio hilo lilitokea jana saa 1:00 asubuhi kwenye nyumba ya shule alimokuwa anaishi mwalimu huyo.

Aidha ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, kutoa elimu kwa wananchi ili kukomesha matukio hayo ambayo yamekuwa yakigharimu maisha ya watu na akasisitiza kuwa hataki kusikia tena mauaji ya kikatili kama hayo.