
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera, John Joseph.
Akizungumza na EATV Mkuu wa TAKUKURU mkoani Kagera, John Joseph, amesema kuwa mfanyakazi huyo wa TANESCO ambaye ni fundi, alitenda kosa hilo kati ya mwezi Machi na Aprili mwaka huu, katika kijiji cha Ruzinga kata Bugene wilayani Karagwe.
Joseph amesema kuwa mfanyakazi huyo alifanikiwa kuiba nguzo ya shirika hilo na kuipeleka kwa mwananchi huyo na baadaye TANESCO waligundua uwepo wa nguzo kinyume cha taratibu na kutoa taarifa TAKUKURU ambao walianza uchunguzi.