Ijumaa , 27th Jan , 2023

Mwili wa Mtanzania Nemes Tarimo aliyefariki dunia akipigana vita nchini Ukraine upande wa Urusi utaagwa hii leo jijini Dar es Salaam, na utasafirishwa kupelekwa Kijiji cha Kasyeto Tukuyu mkoani Mbeya, kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho Januari 28, 2023.

Nemes Tarimo

Mwili wa Nemes umewasili nchini Tanzania asubuhi ya leo Januari 27, 2023, na alifariki dunia Oktoba 24, 2022.

Waombolezaji wa msiba wa Nemes uliopo Kimara Dar es Salaam

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax, Mtanzania huyo alikwenda nchini Urusi mwaka 2020 kwa ajili ya masomo ya shahada ya uzamili katika fani ya biashara, lakini mwezi Machi 2022 alipatikana na hatia ya uhalifu na kuhudukumiwa kifungo cha miaka 7 na umauti ukamkuta  Oktoba 24, 2022 akiwa vitani.