Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga, na kusema kuwa Juni 30 mwaka huu mtuhumiwa huyo ambaye ni msanii wa sanaa ya uchoraji alijirekodi video fupi akitamka maneno makali ya kumkashifu Rais Samia huku akichoma picha inayomuonesha Rais na kuisambaza mitandaoni.
Mapema leo asubuhi Julai 2, 2024, Mkuu wa mkoa wa Mbeya, alitoa saa 24 kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo kuhakikisha kwamba kijana huyo anakamatwa kwani kitendo alichokifanya si cha kimaadili wala kiungwana na kiko tofauti na utamaduni halisi wa wakazi wa mkoa huo.