Alhamisi , 17th Feb , 2022

Aliyewahi kuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amesema kwamba amefurahishwa na kitendo cha Rais Samia kukutana na Tundu Lissu nchini Ubelgiji na kuamini kwamba wamejadili kwa kina hali ya nchi ya Tanzania.

Rais Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Lema ameandika ujumbe huo na kusema.

"Nimefurahi Rais Samia Suluhu Hassan, kukutana na Makamu Mwenyekiti wetu Tundu Lissu, kukutana kwao kunajenga matumaini katika siku za usoni, ninajua  watakuwa wamejadili kwa kina hali ya nchi yetu na changamoto zake kwa sasa na njia nzuri ya kuzivuka," ameandika Lema.