
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 22/ 2023 katika mtaa wa 14 Kambarage Halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita
Mama mzazi wa mwanamke aliyejeruhiwa sio mara ya kwanza kwa wawili hao kugombana na wamekuwa wakipatanishwa mara kadhaa
"Walishawahi kugombana akaja nyumbani Mkwilima nikawasuluhisha wakarudi nyumbani sasa jana ndo napigiwa simu mtoto wako kachomwa kisu na mkwe wako amejinyonga" amesema Anastazia Paul Mama mzazi wa Majeruhi
Baadhi ya majirani wa wawili hao wameeleza kuwa walipigiwa simu na kuelezwa kuwa kuna mtu kajinyonga ndipo walipokutana na mkasa mzima
"Tukio la mke na mume wake kukatana mapanga tulilijua baada ya kupigiwa simu kuwa kuna mtu kajinyonga tukafika ndani nikakuta mmoja hajafa nikafika nikamuita jina akaniangalia na akaninyoshea mkono ndo nikatoka nje haraka nikawambia kumbe dada huyu hajafa ndo wakaja wakampeleka hospitalini na mpaka sasa tupo hapa hospitali tunamhudumia" - amesema Editha Lufungulo ambaye ni Jirani wa Marehemu.
Dkt Salumu Mfaume ambaye ni Mganga mfawidhi hospitali ya Mkoa wa Geita amesema mnamo Novemba 22 mwaka 2023 walipokea mwanamke mwenye umri wa miaka 34 mkazi wa Geita majira ya saa tano hasubuhi katika idara ya dharura alikuwa na majeraha mbalimbali kwenye mwili kwenye mikono, kwenye shingo na Mabegani
Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Geita ACP Adam Maro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada ya mwanaume huyo kukagua simu ya Mke wake.
"Nikweli kuna tukio hilo limejitokeza na tumepata taarifa kutoka kwa bwana Colini mtendaji wa mtaa wa 14 kambarage kwamba kuna mwananchi amejinyonga kwamba walikuwa na ugomvi na mkewe na ni kweli timu ya polisi ilifika na majira ya saa sita kasoro walikuta ni kweli mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Martine John alimaarufu kama alikona ambaye ni mkulima wa Buhalahala na ni mpiga debe wa stendi kuu wa Geita walikuta amejinyonga katika chumba alipokuwa amepanga na Mkewe" amesema Adam Maro ambaye ni Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita.