Treni iliyopata ajali
Ajali hiyo imetokea saa 6:30 usiku wa kuamkia leo kwa saa za Afrika Mashariki ikihusisha treni ya mwendokasi ya Indore-Patna Express, ambapo takriban mabehewa yake 14 yaliacha njia na kupinduka.
Taarifa zinasema kuwa wengi walioathirika zaidi ni abiria katika mabehewa mawili yalikuwa karibu na injini, ambayo yalipinduka kabisha na kusababisha miili ya airia hao kuharibika vibaya.
Eneo la tukio
Abiria mmoja ambaye alikuwa katika behewa ambalo halijakumbwa na kadhia hiyo, ameliambia Shirika la Habari ya Associated Press kuwa treni hiyo ilikuwa ikienda kwa mwendo wa kawaida, lakini ghafla ilisimama na kuanza tena mwendo, dakika chache kabla ya ajali kutokea.
Kazi ya uokoaji inaendelea na huenda vifo vikaongezeka, huku askari zaidi ya 250 wakiwepo eneo la tukio.