Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla
Akizungumza wakati akipokea msaada wa Madati 400 kutoka kwa Kampuni ya uchimbaji wa Madini ya Panda hili Tanzania Limited ambayo inatarajia kuanza kuchimba Madini adimu Duniani aina ya NIOBIUM, amesema Wilaya ya Mbeya ni miongoni mwa halmashauri sita zilizokamilisha zoezi la utengenezaji wa madawati.
Makala amesema kuwa jiji la Mbeya limeshindwa kukamilisha zoezi hilo kwa muda uliopangwa kwa sababu lilielekeza tenda kwa chuo cha Ufundi VETA pekee.
Makala amesema halmashauri hizo zina ziada ya Madawati na kwamba jiji la Mbeya kwa kushirikiana na ofisi yake wamehamisha Tenda kwa mtu Mwingine ambaye atafanya zoezi hilo kwa muda mfupi.





