Alhamisi , 8th Aug , 2024

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Deus Sangu, ameonya tabia ya baadhi ya maafisa utumishi na maafisa tawala kutoa ushauri kwa lengo la kuwafurahisha wakuu wao badala ya kusimamia miongozo ya kazi zao hali inayopelekea ushauri huo kuwaumiza baadhi ya watumishi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Deus Sangu,

Amesema tabia hiyo ya kujipendekeza imejengeka miongoni mwa maafisa utumishi na maafisa tawala hao ya kutaka kuonekana wao ni wema na wasiotaka kuwakwaza wakuu wao muda wote

Mhe. Sangu ametoa kauli hiyo leo kwenye kikao kazi cha watumishi wa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa mara baada ya kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi, ikiwa ni ziara ya kwanza kuzungumza na watumishi tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo.

Amesema tabia hiyo imewaumiza watumishi wengi kwani muda mwingi hutoa ushauri ambao ni kinyume cha haki na wajibu wa utumishi.

Katika hatua nyingine Mhe. Sangu amezitaka mamlaka za ajira na nidhamu kusimamia haki na stahiki zote za watumishi huku akizionya Mamlaka hizo kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea