Ijumaa , 9th Sep , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge ametangaza tarehe rasmi itakayofanyika Wiki ya Uwekezaji Pwani ambapo maonyesho hayo yatatoa taswira ya wepesi na urahisi kwa wawekezaji kuwekeza ndani ya Mkoa wa Pwani.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge

Akizunzungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano uluofanyika leo Septemba 9 kwenye Ukumbi wa mikutano uliopo Wilayani Kibaha Mkoani hapa amesema kuwa hivi sasa baadhi ya wawekezaji wamekua wakiishi ndani ya Mkoa kutokana na kuwawekea mazingira mazuri ya kuishi.

Amesema kuwa maonyesho hayo yatafanyika kuanzia Oktoba 5 hadi 10 mwaka huu ambapo yatafanyika kwenye viwanj vya stendi ya zamani ya Mailimoja Kibaha.

Amesema kuwa Mkoa tayari umefanya maandalizi ya kutosha pia wanatarajia kuwa maonyesho hayo yatafunguliwa na Kiongozi mkubwa kutoka serikalini.

"Wiki ya Biashara na Uwekezaji imepangwa kuzinduliwa rasmi Oktoba 6, 2022 na inatarajiwa kushirikisha washiriki 520 na kukadiriwa kupata watembeleaji 15,000." amesema RC Kunenge.