Hayo yamesema na Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina wakati wa uelimishaji Wananchi na Wafanyabiashara Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita na kuhudhuriwa na Wenyeviti wa Serikali za vijiji, Kata na Halmashauri,ambapo amesema Wilaya ya Mbogwe inaongoza kwa ufanyaji wa Biashara holela ya mafuta ikiwemo ile iliyo maarufu kwa jina la kupiga nyoka kitu ambacho ni kosa kisheria na hatari kwa usalama wa Wananchi.
Kwa upande mwingine, Mhina amewaomba wananchi kuchangamkia fursa ya kuuza mafuta kwa kuomba leseni kwani kwa kanda ya ziwa EWURA imetoa leseni 575 na kati ya leseni hizo 26 wamiliki wamepewa barua za kujieleza ndani ya siku saba baada ya kubainika hawatoi huduma.