Ijumaa , 25th Nov , 2022

Mamlaka ya mapato nchini Tanzania TRA kupitia chuo chake cha kodi imewataka wahitimu waliomaliza kozi mbalimbali za kikodi katika Mahafali ya 15 kwenda kuzingatia elimu ya Kodi ili kupunguza uhitaji wa watalaam uliopo serikalini na sekta binafsi.

Mkuu wa Chuo cha kodi Prof Isaya Gairo

Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Laurence Mafuru ambaye amewataka watalaam Hao kuwa chachu katika kuongeza pato la serikali kwa weledi kwenye utendaji wao.

'Kupitia mafunzo haya nendeni mkawe chachu katika kushauri kutenda na kuikataa rushwa mkaifanye azma ya serikali kwenye utendaji wake kufikia kirahisi mapinduzi ya viwanda kafanyeni kazi kwa weledi mkitanguliza maadilim ya kikodi'Amesema Mafuru

Pamoja na hilo amewataka pia kuhakikisha wanawekeza katika maadili yenye kuikataa rushwa ili kuhakikisha azma ya serikali kwenye mapinduzi ya viwanda inafikiwa pakiwa na wataalamu wa kikodi

Katika mahafali hayo mkuu wa chuo cha kodi prof Isaya Gairo amesema wahitimu ni 489 wa kike wakiwa 198 wanaume 291 akidai kuwa wahitimu hayo wanaweza kuongeza kasi kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani serikalini ama kupitia sekta binafsi.

Kwa pande wao wahitimu waliofanya vizuri kwa ufaulu wa juu katika masomo wamesema siarir ya ushindi nim kujituma kupenda unachokifanya wakiahidi kwenda kufanyia kazi ushauri na utalaamu waliopatiwa.