Alhamisi , 16th Mar , 2023

Zaidi ya wakazi 1800 katika kata ya mabwepande mkoani Dar es salaam wameanza sasa kulipia maeneo yao kwa ajili ya kuandaliwa hati na kumiliki ardhi kisheria mara baada ya kuzinduliwa kwa zoezi la utoaji wa namba maalum yaani control namba sambamba na kutoa barua za utambulisho.

Zoezi la ulipaji wa ardhi limezinduliwa rasmi kata ya Mabwepande

Zoezi la Kuwapatia nammba na barua Maalum linatokana na kukamilika kwa Zoezi la Upimaji Ardhi lililokuwa likiendeshwa na Shirika la Maendeleo la DDC mkoa wa Dar es salaam kwa wakazi hao waliovamia ardhi inayomilikiwa na Shirika hilo ambapo baada ya Makubaliano na Serikali ya Mkoa Dsm wananchi hao walikubali kulipa shilingi 6500 kwa Square Mita Moja.

Baadhi ya Wananchi wamelipokea zoezi hilo kwa furaha kwa kuwa linakwenda kumaliza Migogoro ya Ardhi iliyodumu katika kata ya Mabwepabde kwa zaidi ya Miaka 20 lakini pia kupata Umiliki halali wa Ardhi kupitia hati watakazopata huku wakishukuru serikali kupiti a shirika hilo