Jumamosi , 25th Jun , 2022

Baadhi ya wafanyabiashara, waliohamishwa kutoka soko Bati  na kupelekwa soko  jipya la Chuno, katika  Manispaa ya Mtwara Mikindani, wamewaomba viongozi wa serikali kuweka utaratibu utakaomuwezesha kila mfanya biashara aliyehamia sokoni hapo kupata eneo la kufanyia biashara zao.

Wakizungumza sokoni hapo, wafanyabiashara  hao wamesema, licha ya kuhamia sokoni hapo,   baadhi yao wanadai  kukosa maeneo  kufanya biashara.

Kwa upande wake katibu wa soko hilo,  chigwalu issa, akaeleza uwezo wa soko hilo na wafanyabiashara ambao tayari wamepokelewa sokoni hapo.
Soko kuu la kisasa la chuno  lilijengwa kwa shilingi bilioni 5.3, na kuzinduliwa rasmi desemba 2020.