Jumanne , 19th Apr , 2022

Baadhi ya wafanyabiashara na wabunifu wamesema ni vyema sasa serikali ikaangalia maeneo ikiwezekana Kila Wilaya pakatengwa eneo maalamu Kwa ajili ya kuuza bidhaa za wabunifu Ili kutoa fursa kukuza vipaji vyao lakn pia Kuongeza Kodi ya Serikali.

Hayo yamebainishwa na wafanyabiashara pamoja na wabunifu wa bidhaa mchanganyiko wakiwemo wachongaji,mafundi wa samani,wachomeleaji ambao wamesema uwepo wao unaongeza mnyororo wa  thamani hivyo sasa kuiomba kupitia Halimashuri zake kukawepo eneo maalamu Kwa wabunifu kama ilivyo Kwa wajasiriamali na wamachinga.

"Sisi tuko na ujuzi Mimi nikichonga ama kutengeneza jiko likawa tayari nimehusisha watu wengi ambao kupitia Mimi wamepata pesa hivyo haya mazingira ambayo serikali inaweka iwekeza sasa kwetu Ili tuone vipaji vingi zaidi vikikua kibiashara tuweze kuwa na soko la ushindani." Alisema Khatibu Mashana -Mbunifu.

Kuhusu mazingira ya Uwekezaji na uwezeshaji wamesema mtu yeyote anatamani kupata eneo lenye utulivu ili aweze kuzalisha bidhaa tofauti na ilivyo sasa wanaofanya pembezoni mwa barabara hudaiwa kuondolewa na mamlaka za serikali ikiwemo TANROADS.

"Tunatamani Sana kufanya uwekezaji lakini haya mazingira siyo mazuri Sana kutokana na Mara nyingi maeneo haya tumepanga tuu bidhaa hatujarasimishwa"alisema Said Hadsani-Mfanyabiashara/Mchongaji.

Kwa Jiji la Dar es Salaam  wapo vijana wengi mitaani ambao hufanya shughuli zao za kujiingizia kipato hivyo endapo watarasimishwa serikali itapata mapato kupitia kazi zao.