Wafanyabiashara hao wamesema tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi kwao unafuu fulani umekuwepo kibiashara kutokana na watu kupata nafasi ya kuzunguka huku na huko ukilinganisha na kipindi ambacho watu wametoka katika corona.
"Afadhali kwa sasa biashara inaenda tukienda kwenye mikutano hatutoki kapa maana ndipo waetja walipo iendelee tu tuone na viongozi watakaoshinda watakuja na sera gani za kutusaidia sisi wapiganaji mtaani" amesema mmoja wa wafanyabiashara hao.
Akizungumzia utofauti uliopo wa kampeni zilizopita na sasa mmoja ya wafanyabiashara hao amesema kikubwa ni watu kuangalia jinsi wanavyoweza kutumia fursa hizo chache zinazojitokeza katika kipindi hiki.
Matarajio ya wafanyabiashara wengi wa bidhaa mbalimbali ni kukutana na fursa nyingi za kibiashara mara baada ya kuanza kwa kampeni za vyama vya siasa hali ambayo mpaka sasa bado haijaonesha kuchangamka sana.