
Mkurugenzi wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodgar Tenga.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodgar Tenga wakati akitangaza kuhusu shindano la Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora wa mwaka ikiwa na lengo la kutambua makampuni yanayohusika na uzalishaji wa bidhaa na huduma nchini.
“Kwa kipindi chote tumepata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau mbalimbali na kwa mwaka huu tumekwisha pokea idadi kubwa ya washiriki kutoka viwanda mbalimbaoi kote nchini. Tunahamashisha makampuni mengi kushiriki na hususani tunahamasisha ushiriki wa viwanda vya kati na vidogo” alisema Bw Tenga
Tenga amewataka viwanda vya kati na vidogo kutumia jukwaa hilo kama nafasi ya kwao kuongoza kwenye nyanja tofauti ili kuweza kutambulika, kuchangia ukuaji wa biashara zao huku washiriki wakieleza manufaaa waliyopata katika mashindano 15 yaliyopita.
“Mbuyu ulianza kama mchicha , hivyo ni muda muafaka kwa viwanda vya kati na vidogo kutumia jukwaa hili kama nafasi kwao kuongoza kwenye nyanja tofauti kutambulika, kuchangia ukuaji wa biashara zao”aliongeza Tenga