Jumatano , 9th Nov , 2022

Maznat Beuty College kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imefanikiwa kuwafadhili  vijana mbalimbali kutoka mtaani na kufanikiwa kuhitimu mafunzo ya ujasiriamali na urembo ambapo mafunzo hayo yatawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuweza kujiajiri ili kuepuka utegemezi.

Hayo yamesemwa katika mahafali ya chuo cha ujasiriamali na urembo (Maznat Beauty College) ambapo Mkurugenzi Mkuu Maznat amesema kuwa Chuo hicho kwa kushirikiana na  wadau wenginee wamefanikisha mafunzo ya ujasiriamali na urembo kwa vijana ambao watakuja kuinuka kiuchumi, kujiendeleza kibiashara na kuinua wengine ili kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira.

Kwa upande wake Mwakilishi  wa Mkuu Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe amesema kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono vijana na kuwawezesha ili waweze kuinuka kiuchumi.