Alhamisi , 21st Apr , 2022

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekutana na wataalam wa kampuni ya Meta inayomiliki mtandao wa instagram, whatsapp na facebook kujadili namna ya kukusanya kodi kupitia huduma zao nchini.

Kwenye picha ni wataalam wa kampuni ya Meta wakiwa na viongozi wa TRA.

TRA imefanya mazungumzo ya awali na kampuni ya Meta kuhusu namna ya kutoza kodi katika huduma zao nchini. Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.

TRA wametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wao wa twitter.