
Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha wakati waandishi wa habari za kiuchumi, biashara na uwekezaji walipotembelea bandari hiyo na kujionea maboresho yanayoendelea katika bandari hiyo.
Meneja Mrisha amesema serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), inatekeleza mradi huo mkubwa wa kimakakati wa maboresho makubwa katika bandari ya Tanga ili iweze kuchangia kikamilifu katika kukuza pato la Taifa kwa kuhudumia wateja wa ndani na nchi jirani ambazo zinategemea bandari za Tanzania kusafirisha bidhaa kutoka na kwenda nje ya nchi.
"Mikakati yetu ya kimasoko baada ya kukamilika kwa ujenzi huu ni pamoja na kuitangaza bandari ya Tanga kwa kutumia vyombo vya ndani kama Radio na luninga na kuonyesha makala maalumu nje ya nchi kwa kutumia watumishi wa bandari waliopo nchi tunazohudumia, pamoja na Balozi zetu nchi mbalimbali kuitangaza bandari," amesema Mrisha.
Kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika mradi wa maboresho ya bandari hiyo mradi huo utakapokamilika utakuwa na faida mbalimbali ikiwemo uwezo wa bandari ya Tanga wa kuhudumia shehena utaongezeka kutoka tani 750,000 mpaka tani 3,000,000.