
Kampeni ya Patapata inayoendeshwa na kampuni ya Tigo
Akizungumza na waandishi wa habari leo usiku, Meneja Uendeshaji wa The Network, Lumuliko Mengele amewataja washindi wawili wa mchezo huo kuwa ni Mathias Januari mkazi wa Dodoma na Urembo Yusuph mkazi wa Dar es salaam.
Washindi hao wawili wa mchezo wa patapata wamefanikiwa kujishindia shillingi million tano kila mmoja.
Aidha Meneja Biashara wa Tigopesa, Ibrahim Mfala amewahamasisha wateja na watumiaji wa mtandao wa Tigo kuendelea kucheza mchezo hyo ili waweze kushinda.