Jumapili , 5th Feb , 2023

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Lazaro Kilahala ametoa wito kwa Taasisi za Umma na Serikali zinazodaiwa na Wakala huo baada ya kupatiwa huduma za matengenezo ya magari, mitambo, huduma za ufundi, umeme na elektroniki, kuilipa TEMESA madeni inayowadai

Kilahala ametoa wito huo wakati akizungumza katika kikao cha Wadau wanaopatiwa huduma na TEMESA Mkoa wa Dodoma, kikao kilichofanyika jijini Dodoma ambapo kikihudhuriwa na maafisa wanaowakilisha Taasisi za Umma wakiwemo maafisa usafirishaji, maafisa kutokaSerikali kuu, Wizara mbalimbali, wawakilishi wa karakana teule zinazofanya kazi kwa pamoja na TEMESA pamoja na wazabuni wanaosambaza vipuri na vitendea kazimbalimbali kwa Wakala huo.

Mtendaji Mkuu amesema, anafahamu changamoto ambazo wanakutana nazo kwenye Taasisi na Wizara zao ikiwemo kutokutosha kwa mgawanyo wa fedha za maendeleo akiwataka kulipa uzito suala la kulipa madeni yao kwa TEMESA Kwani kutowalipa TEMESA kwa wakati kutasababisha ishindwe kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa kukosa vipuri vya kuwatengenezea magari ya Taasisi zao na hivyo kurudisha nyuma maendeleo.