Jumatano , 12th Oct , 2022

Imeelezwa kuwa moja ya changamoto ambayo imekwamisha Kwa kipindi kirefu sekta za uzalishaji kukua kutofungana Kwa sera za nchi baina  ya sekta na sekta Hali ambayo imesababisha kuzorota sekta za uzalishaji.

Hayo yamebainishwa na Naibu waziri wa uwekezaji viwanda na Biashara Exaud Kigahe katika majadiliano ya pamoja Watalaamu wa uchumi na kisera kutoka nchi 11 pamoja na washirika wa maendeleo kutoka umoja wa mataifa ambapo ishu kutofungamana Kwa sera changamoto za uzalishaji duni kwenye sekta za Kilimo zinakwamisha viwanda ambayo ndiyo azma  ya Serikali.

Amesema Kwe ishu ya uzalishaji nchi imekuwa nyuma Kwa kipindi kirefu ambapo sasa wanahuhisha baadhi ya sera ziendane na wakati uliopo.

Hata hivyo Watalaamu kutoka mashirika binafsi, wataalamu wa utafiti wamebainisha changamoto nyingi ziko kwenye sekta ya Kilimo, viwanda, ujenzi,sukari na mafuta ya kula.

Mkutano huo umebainisha matatizo mengi ya Africa ni umasikini hivyo kuja sasa na sera na mikakati ya kuinua uchumi ukiwemo mradi huo ambao umeanzishwa tangu mwaka 2020 Tanzania ikiwa ni mnufaika.