Jumatatu , 26th Aug , 2024

Serikali nchini inatarajia kutangaza afursa za kiuchumi kwa wawekezaji ndani na nje ya nchi zitokanazo na mazingira ili kuokoa maliasili ambazo zimekuwa zikiharibiwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dkt.Ashatu Kijaji

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dkt.Ashatu Kijagi, wakati anaongea na wanahabari kuhusu maandalizi ya  mkutano wa viongozi, wataalam na wadau kuhusu uhifadhi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

"Mkutano utajadili fursa zilizopo katika hifadhi na usimamizi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi. Hii ni pamoja na Biashara ya Kaboni; usimamizi wa taka; mabadiliko ya tabianchi; nishati safi ya kupikia; upandaji miti na usimamizi na uzingatiaji wa Sheria nchini", Dkt. Ashatu  Kijaji , Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Aidha Dokta Kijagi anaelezea athari za uharibifu wa mazingira ulivyoathri nchi yetu kiuchumi.

"Uharibifu wa ardhi,  uharibifu wa vyanzo ya maji, ukataji miti ovyo na uharibifu wa misitu; upotevu wa makazi ya wanyamapori na bayoanuai; athari za mabadiliko ya tabianchi; uharibifu wa mifumo-ikolojia ya pwani na baharini; uharibifu wa ardhi oevu; uchafuzi wa mazingira; na kuenea kwa viumbe vamizi", Dkt. Ashatu  Kijaji , Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Nao wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam wanatoa maoni mseto kuhusu maeneo ambayo wangependa Serikali iweze kuangazia kwa undani zaidi.

"Kama ambavyo tunaona mvua zikipungua wakulima wanakosa mazao na kushindwa kuzalisha, basi waweke kampeni maalum itakayoongeza nguvu kwenye upandaji miti ili tuweze kupata mvua za kutosha na wakulima waweze kuzalisha kwa wingi na nchi ytu itabaki salama", Yasin Sheshe, Mkazi wa Dar es Salaam.

"Nchi yetu ina Umeme wa kutosha ina Gesi, huenda wataalam wa kutosha hakuna lakini ikitenga bajeti kwa ajili ya kuwasomesha wataalam ambao watakuja kufanya kazi kwenye miundombinu yetu na baadae tutaondokana na matumizi ya nishati zisizo salama", Zakayo Mathayo, Mkazi wa Dar es Salaam.

"Mimi ningetamani viongozi watakaoshiriki mkutano huo kwanza kabisa waanze na mazingira yetu ya kila siku mfano Dar es salaam, hapa utatembea mita 200 hyaukutani hata na dustbin kwahiyo wangeanza udhibiti sasa hivi kwenye maeneo ya mjni halafu vijijini naimani tutafanikiwa sana kwenye mazingira yetu" ,Noel Kisubi, Mkazi wa Dar es salaam.