Alhamisi , 8th Jun , 2023

Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kusambaza,kununua vifaa vya nishati mbadala ambavyo itavisambaza nchi nzima ili kutimiza azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama kuni kichwani.

Waziri wa Nishati January Makamba

Kauli hiyo imetolewa na waziri wa Nishati January Makamba wakati mafunzo ya Namna ya kutumia Nishati mbadala kwa mama lishe na vijana yaliyolenga kuongeza tija katika uzalishaji huku mwenyekiti wa mtandao wa kukuza wanawake kiuchumi TAWEN akiwataka sasa wajasiriamali kuuvaa uhusika kamili katika mazingira

Baadhi ya wadau wa nishati mbadala mama lishe na vijana wamesema mpango huo utawasaidia kina mama wengi kuondokana na ukatili ambao umekuwa ukiwapata kutokana na kutafuta kuni maporini huku familia wakiwa wameziacha nyumbani kwa muda mrefu.

Nae Mtaalamu wa Nishati mbadala ameitaja sekta hiyo kama mwokozi wa rasilimali mbalimbali kama miti huku ikichagiza uzalishaji kwa kipindi chote iwe mvua ama jua mama lishe na vijana wajasiriamali watakuwa na uwezo wa kufanya kazi zao kwa weledi zaidi.