Jumatatu , 26th Feb , 2024

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye bidhaa ya sukari ili kuwasaidia wananchi kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kutopanda bei ya bidhaa hiyo.

Rais Dkt. Mwinyi akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Jumbi leo Februari 26, 2024 wakati wa ziara yake ya kusikiliza changamoto zao

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Jumbi na Soko la samaki Malindi Mkoa wa Mjini Magharibi Februari 26, 2024 katika ziara yake maalumu  ya alipotembelea masoko na  kusikiliza changamoto zao. 

Aidha, Dkt. Mwinyi amewaomba wafanyabiashara kutopandisha bei ya vyakula kiholela bila ya sababu za msingi kwa kupandisha mara mbili ya bei ili kuwasaidia wananchi wanyonge kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.