
Wakizungumza na EATV wafanyabishara hao wa soko la Mwananyamala Mapinduzi jijini Dar es Salaam wamebainisha kuwa mvua inayoendelea kunyesha katika meneo mbalimbali nchini imekuwa ikiathiri bei ya nafaka sokoni, hususani maharage kutokana na usafirishaji wake kuwa wa juu na kuharibika pindi inaponyeshewa na mvua.
Aidha, Mwenyekiti wa Soko hilo Mwananyamala Mapinduzi Mbaraka Salum amebainisha kuwa serikali inapaswa kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara katika maeneo yanapotoka mazao hayo ili kurahisisha nafaka hiyo kushuka bei yake.