Ijumaa , 27th Mei , 2022

Baadhi ya wakulima wa Kahawa na mazao mengine ya Biashara ikiwemo Pamba, Korosho na Kahawa wamesema zoezi la ukaguzi wa mizani  linalondeshwa na wataalam kutoka wakala wa vipimo nchini limelenga kuleta usawa kati ya muuzaji na mnunuzi.

Rai hiyo imetolewa na wakulima hao wa kahawa ambao wanakwenda kuanza rasmi msimu wa kahawa Juni mosi ,2022 wakieleza wamekuwa wakipoteza hadi kilo 300 kwa tani moja kutokana na wanunuzi kutumia mizani iliyochezewa.

Kwa mkoa wa Kagera takribani. zaidi ya mizani 300 ya wanunuzi wa kahawa inategemea kuhakikiwa kabla na kwamba ni jukumu la wakala  kufanya ukaguzi kabla ya msimu kuanza ili kuridhisha pande zote katika biashara.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa wakala wa vipimo nchini WMA Stella Kahwa amesema Lengo ni kuifikia mikoa yote inayokwenda katika msimu wa kuuza mazao ikiwemo Kagera, Shinyanga, Mtwara ili kuhakikisha mazingira ya kiuwekezaji yanafikiwa.